Thursday, March 8, 2012
MESSI APIGA TANO BARCA IKISHINDA MABAO 7-1.
MSHAMBULIAJI wa Barcelona Lionel Messi ameweka historia mpya katika michuano ya Klabu Bingwa Ulaya baada ya kufanikiwa kufunga mabao matano wakati timu yake ikiibuka na ushindi wa wa mabao 7-1 dhidi ya Bayer Liverkusen. Mabingwa hao watetezi walifanikiwa kushinda mchezo huo na kufanikiwa kutinga hatua ya robo fainali kwa kishindo kwa jumla mabao 10-2 huku Messi akiweka historia ya kuwa mchezaji wa kwanza kushinda idadi hiyo ya mabao katika michuano hiyo. Akihojiwa mara baada ya mchezo huo kocha wa Leverkusen Robin Dutt alisifia kiwango cha timu ya Barcelona akisema kuwa timu inapocheza bila Messi inakuwa bora lakini kama anakuwepo uwanjani timu inakuwa ni kama imetoka sayari nyingine. Kocha wa Barcelona Pep Guardiola pia alimsifu mshambuliaji wake huyo kwa kiwango alichokionyesha akisema kuwa hakutawahi kutokea mchezaji huko siku za mbele mwenye kiwango cha kipekee kama Messi. Mshambuliaji huyo bora wa dunia mara tatu alifunga mabao yake katika dakika 25, 42 na 49 na kutimiza idadi ya kufunga mabao matatu mfululizo-Hat Trick mara 17 akiwa na klabu ya Barcelona kabla ya kuongeza mengine mawili dakika ya 58 na 84 ya mchezo huo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment