Sunday, March 18, 2012

MESSI, XAVI WAIPAISHA BARCELONA.

MABAO ya Xavi aliyefunga kwa mpira wa adhabu na lingine la Lionel Messi yalitosha kuipa Barcelona ushindi wa 2-0 jana dhidi ya Sevilla na kupunguza idadi ya alama wanazozidwa na Real Madrid. Xavi alipiga bao hilo dakika ya 18 na Mwanasoka Bora wa Dunia, Messi akafunga bao lake la 31 kwenye La Liga msimu huu baadaye kidogo. Mabingwa hao watetezi sasa wana pointi 63 kutokana na mechi 27, wakati Jose Mourinho ameiweka kileleni kwa mbali Real, yenye pointi 70 na leo inaweza kutudisha pointi 10 za kuizidi Barca iwapo itashinda dhidi ya Malaga Uwanja wa Bernabeu. Katika mechi nyingine, Osasuna ilipanda hadi nafasi ya tano kwa kufikisha pointi 39 baada ya kupata bao la kusawazisha dakika za lala salama na kufanya sare ya 1-1 na Real Zaragoza.

Rayo Vallecano ilipanda hadi nafasi ya nane kwa kufikisha pointi 37 baada ya kuifunga Real Betis 3-0. Zaragoza inabakiwa nafasi ya 20 kwa pointi zake 19.

1 comment:

  1. Hi, cool post. I have been thinking about this topic,so thanks for sharing. I will probably be subscribing to your blog. Keep up great writing!!!
    2009 Jeep Wrangler AC Compressor

    ReplyDelete