NEW HEAD OF BRAZILIAN FOOTBALL WANTS FEW CHANGES.
|
Jose Maria Marin |
KIONGOZI mpya wa Shrikisho la Soka la Brazil aliyechukua madaraka hayo jana ameahidi kufanya mabadiliko machache licha ya mara nyingi utawala wa aliyemtangulia Ricardo Teixeira kukumbwa na utata. Jose Maria Marin ambaye ni mwanasiasa ndiye aliyechukua nafasi ya Teixeira ambaye alijiuzulu Jumatatu kutokana na matatizo ya kiafya aliyonayo baada ya kuongoza shirikisho hilo kwa miaka 23. Akizungumza mara baada ya kuchukua wadhifa huo Marin amesema kuwa uongozi wa Teixeira ni wa kuigwa kwakuwa amefanya soka la nchi hiyo kutambuliwa duniani kutokana na juhudi zake. Teixeira alifufua shirikisho hilo katika kipindi chake lakini pia alikuwa akituhumiwa na rushwa na ukiukwaji wa wa taratibu katika uongozi wake. Marin ambaye ana umri wa miaka 79 ataliongoza shirikisho hilo mpaka mwishoni mwa 2014 baada ya Kombe la Dunia ambalo nchi hiyo ndio itakuwa mwenyeji ambapo ameajidi kuwa tayari kwa mazungumzo na serikali ili kuhakikisha maandalizi ya michuano hiyo yanakwenda kama yalivyopangwa.
No comments:
Post a Comment