Tuesday, March 20, 2012

RONALDO AITAMANI NAFASI YA URAIS CBF.

NYOTA wa zamani wa Brazil Ronaldo de Lima ambaye kwasasa ni mjumbe wa Kamati ya Maandalizi ya Kombe la Dunia nchini Brazil 2014 ameonyesha nia ya kugombania nafasi ya urais wa Shrikisho la Soka nchini humo. Akinukuliwa na gazeti maarufu nchini humo liitwalo Folha de Sao Paulo Ronaldo amesema kuwa angependa kuanza zake za kisiasa katika soka na anahitaji kuongoza soka hivi sasa baada ya kucheza kwa kipindi kirefu. Aliyekuwa rais wa CBF Ricardo Teixeira ambaye ameliongoza shirikisho hilo kuanzia mwaka 1989 alijiuzulu wadhifa wake huo kutokana na matatizo ya kiafya na pia alijiuzulu nafasi ya ujumbe katika kamati ya maandalizi ya nchi hiyo. Katika kipindi cha miaka 22 ambacho Teixeira ameliongoza shirikisho hilo alikuwa amejitahidi kukuza soka la nchi hiyo lakini katika kipindi cha karibuni kabla ya kujiuzulu CBF imekuwa ikikumbwa na shutuma mbalimbali za uadilifu. Ronaldo ambaye alikiongoza kikosi cha nchi hiyo kunyakuwa taji la Kombe la Dunia mwaka 2002 amesema kuwa hajajua kama atakuwa mgombea wa nafasi ya urais lakini kama CBF wakimhitaji kufanya hivyo atakubali kugombea.

No comments:

Post a Comment