Thursday, March 8, 2012
RONALDO ATETEA KAULI YA VALCKE.
MCHEZAJI nguli wa zamani wa Brazil Ronaldo de Lima amekiri kuwa Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA Jerome Valcke alikuwa yuko sahihi kuhusiana na matatizo yaliyopo katika maandalizi ya michuano ya Kombe Dunia 2014 nchini Brazil. Valcke aliingia katika mzozo na Wziri wa Michezo wa nchi hiyo Aldo Rebelo kufuatia kauli yake aliyotoa ambayo waziri huyo alisema ni ya kuudhi hivyo kuiandikia barua FIFA kwamba hawatafanya kazi na katibu huyo kwenye tena. Akihojiwa kuhus suala hilo Ronaldo amesema kuwa Valcke tayari ameomba msamaha kutokana na kauli yake hiyo lakini hilo haliwezi kuficha ukweli kwamba alikuwa yuko sahihi alitoa kauli hiyo. Ronaldo ambaye ni mmoja wa wajumbe wa kamati ya maandalizi ya michuano hiyo aliendelea kusema kuwa ni ukweli kwamba nchi hiyo iko nyuma ya muda kuhusiana na suala la miundo mbinu na pia vitu vingi vipo nyuma ya wakati.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment