Wednesday, April 11, 2012

HAVELANGE RECOVERING WELL.

MADAKTARI wamesema rais wa zamani wa FIFA, Joao Havelange anaendelea vizuri baada ya kupatiwa tiba makini ya matatizo ya moyo, baada ya kurejeshwa chumba cha wagonjwa mahututi katika hospitali anayotibiwa nchini Brazil. Taarifa hiyo ya madaktari iliendelea kusema kuwa Havelange mwenye umri wa miaka 95 anaendelea kupata nafuu kutokana na matatizo ya moyo yanayomkabili ambayo yalisababisha athari katika kifundo chake cha mguu wa kulia na kupelekea kulazwa zaidi ya wiki tatu. Daktari anayemhudumia Havelange aitwae Joao Mansur Filho amesema kuwa kama hali yake ikiendelea kutengemaa vizuri kama anavyoendelea hivi sasa basi ataamishwa kutoka katika chumba wa wagonjwa mahututi ingawa hakuweka wazi kama bado ataendelea kutumia mashine ya kupumulia au la. Havelange alilazwa hospitalini hapo toka Machi 18 mwaka huu kutokana na maambukizi ya Bakteria aliyopata katika mguu wake wa kulia ambapo alikuwa akiendelea vyema na matibabu yake kabla ya Jumatatu afya yake kuzorota kutokana na matatizo ya moyo na utu uzima. Havelange alikuwa rais FIFA kuanzia 1974-1998. Alistaafu katika Kamati ya Olimpiki ya Kimataifa-IOC ambayo ameitumikia toka mwaka 1963 mwishoni mwa mwaka jana kwa sababu za kiafya.

No comments:

Post a Comment