MWANASOKA wa zamani wa kimataifa wa Uholanzi, Phillip Cocu ametwaa taji lake la kwanza ikiwa ni siku 28 baada ya kuwa Kocha Mkuu wa timu ya PSV Eindhoven, wakati timu yake ilipoichapa Heracles Almelo mabao 3-0 katika fainali ya Kombe la Uholanzi jana. Cocu, ambaye ni msaidizi wa makocha wa timu ya taifa, Bert van Marwijk, amerithi mikoba ya Fred Rutten aliyefukuzwa mwezi uliopita. Kocha huyo alikataa kupewa sifa zote kwa kuiwezesha timu hiyo kushinda taji kwa kusema kuwa Rutten pia alikuwa na mchango katika mafanikio hayo na sasa wanaelekeza nguvu zao katika Ligi Kuu ya nchi hiyo. Heracles ikicheza fainali ya kwanza ya Kombe la Ligi baada ya kuitoa AZ Alkmaar katika Nusu Fainali, ilionyesha kuzidiwa toka mwanzoni mwa mchezo huo.
No comments:
Post a Comment