Sunday, April 8, 2012
YAYA TOURE KUPUMZIKA KUITUMIKIA TIMU YA TAIFA.
KIUNGO wa Manchester City, Yaya Toure anajipanga kupumzika kuitumikia timu yake ya taifa na kuelekeza nguvu zake kuhakikisha klabu yake hiyo inashinda kombe la Ligi Kuu ya nchini Uingereza msimu ujao. Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ivory Coast alikosa wiki sita za kwanza baada kutoka kutoka kuitumikia timu yake ya taifa katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika Januari mwaka huu. Ambapo kushindwa kwake huko kuitumikia klabu yake hiyo mchezaji huyo mwenye miaka 28 anaamini ni kitu ambacho kimechangia klabu hiyo kupoteza baadhi ya michezo ya ligi pamoja na kutolewa katika Kombe la FA na Kombe la Ligi. Mchezaji huyo wa zamani wa Barcelona alichukizwa na kitendo kocha wa Ivory Coast Francois Zahoui kukataa kuwaruhusu yeye na kama yake Kolo kuchelewa kuondoka klabuni kwa ajili ya michuano ya Kombe la Afrika pamoja na viongozi wa City kumuomba. Yaya ambaye ni mmoja wa wachezaji wanaolipwa zaidi katika klabu hiyo akichukua kiasi cha paundi 200,000 kwa wiki, hivi sasa yuko tayari kuamishia nguvu zake kwa klabu hiyo na yuko katika mpango wa kuongea na viongozi wa City katika kipindi cha majira ya kiangazi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment