Wednesday, May 16, 2012

FERDINAND NJE KIKOSI CHA UINGEREZA.

MENEJA wa timu ya taifa ya Uingereza Roy Hodgson amepanga kumuacha aliyekuwa nahodha wa kikosi hicho Rio Ferdinand kwa ajili ya michuano ya Kombe la Ulaya itakaofanyika mapema mwezi ujao. Ferdinand alithibitisha suala hilo baada ya kuhojiwa na gazeti ya The Sun la nchini humo baada ya kupigiwa na Hodgson kumtaarifu kwamba hakumjumuisha katika kikosi chake cha wachezaji 23 ambacho atakitangaza baadae leo. Kutokuwemo kwa Ferdinand katika kikosi hicho inamaanisha kuwa beki wa Chelsea John Terry anategemewa kusafiri na kikosi hicho katika michuano hiyo uiliyoandaliwa kwa pamoja na nchi za Poland na Ukraine. Kulikuwa na tetesi kuwa Terry nae angeweza kukosekana katika kikosi hicho kutokana na kesi inayomkabili ambayo itasikilizwa Julai mwaka huu ya ubaguzi wa rangi kwa mdogo wake Rio aitwaye Anton Ferdinand tuhuma ambazo Terry mwenyewe amekanusha vikali. Katika taarifa zingine beki wa Tottenham Hotspurs Kyle Walker pia anatarajiwa kutokuwemo kwenye kikosi hicho kutoka majeruhi aliyopata wakati wa mchezo wa mwisho wa Ligi Kuu nchini humo dhidi ya Fulham huku mchezaji wa Liverpool Glen Johnson na Phil Jones wa Manchester United wakitarajiwa kuitwa katika kikosi hicho.

No comments:

Post a Comment