Saturday, May 26, 2012

GUARDIOLA AIAGA BARCELONA KWA KIKOMBE.

KLABU ya Barcelona jana imefanikiwa kutwaa taji la 26 la Kombe la Mfalme au Copa del Rey, baada ya kuifunga Athletic Bilbao mabao 3-0 kwenye Uwanja wa Vicente Calderon katika mechi ambayo kocha wa klabu hiyo Pep Guardiola aliaga rasmi. Barcelona walipata bao la kwanza dakika ya tatu lililofungwa na Pedro wakati bao la pili lilifunga na mshambuliaji nyota wa klabu hiyo Lionel Messi huku bao la tatu lilikifungwa tena na Pedro na kupelekea Guardiola kuipa taji la 14 katika kipindi ambacho amekuwa akiinoa klabu hiyo. Akihojiwa mara baada ya mchezo huo Guardiola aliwashukuru wachezaji wa timu hiyo kwa kumpa ushirikiano mzuri katika kipindi chote alipokuwa hapo na pia kuwashukuru mashabiki na viongozi wa klabu hiyo kwa kumuamini. Guardiola pia alimsifu Messi kwa kusema kuwa imekuwa ni heshima kubwa kwake kumfundisha mchezaji bora kabisa kuwahi kutokea duniani. Kocha huyo ambaye kocha wa kikosi B cha klabu hiyo alichukua mikoba ya kuinoa kikosi kikubwa mwaka 2008 akichukua mikoba ya aliyekuwa kocha wa timu hiyo Frank Rijkaard.

No comments:

Post a Comment