Tuesday, May 15, 2012

MAN CITY WAVUNJA REKODI YA MATANGAZO.


 

KLABU ya Manchester City imeweka rekodi ya kuingiza mapato ya matangazo mengi zaidi katika Ligi Kuu nchini Uingereza baada ya kuingiza dola milioni 97.6 wakati wakinyakuwa taji la ligi hiyo. Tofauti na ligi zingine ambapo mapato hayo hugawiwa vilabu vikubwa, katika ligi ya Uingereza mapato yanayopatikana kupitia luninga za nyumbani pamoja na dunia nzima kwa ujumla huwa yanagawanywa sawa kwa vilabu vyote 20 vinavyoshiriki ligi kuu. Ofisa Mkuu wa ligi hiyo Richard Scudamore amesema kuwa wanaamini mgawo sawa inavyopata klabu zinashiriki ligi kuu inasaidia vilabu hivyo kuwa na ushindani wa hali juu na unaolingana. Kila klabu huwa inapokea kiasi cha dola milioni 22.1 kwa haki za matangazo ya nyumbani na dola milioni 30.1 kwa haki za matangazo ya nje na kiasi cha dola milioni moja kwa kila nafasi waliomaliza katika msimamo wa ligi hiyo. Hiyo inamaanisha Arsenal ambao wamepata dola milioni 90.5 wakati wamemaliza katika nafasi ya tatu lakini Tottenham Hotspurs ambao wameshika nafasi ya nne wao wameweka kibindoni kitita cha dola milioni 92.4 baada ya kucheza michezo 23 iliyorushwa moja kwa moja katika luninga tofauti na mahasimu wao hao kutoka Kaskazini mwa London, Arsenal.

No comments:

Post a Comment