Friday, May 18, 2012
MKONGWE ROGER MILLA AVULIWA URAIS WA HESHIMA CAMEROON.
MCHEZAJI nguli wa zamani wa Cameroon, Roger Milla amevuliwa urais wa heshima aliopewa na Shirikisho la Soka la nchi hiyo-Fecafoot kutambua mchango wake katika nchi hiyo baada ya kuwakosoa viongozi wa shirikisho hilo. Milla ambaye aling’ara katika michuano ya Kombe la Dunia mwaka 1990 aliunda kikundi mwezi uliopita kwa ajili ya kuung’oa uongozi uliopo madarakani wa Fecafoot. Nyota huyo wa zamani alilikosoa shirikisho hilo kutokana na mwenendo mbovu wa kikosi cha timu ya taifa ya nchi nchi hiyo maarufu kama Indomitable Lions pamoja na uamuzi wa kumfungia mshambuliaji nyota na nahodha wa kikosi hicho Samuel Eto’o. Akihojiwa mara baada ya kuvuliwa wadhifa wake huo Milla ambaye ana umri wa miaka 59 amesema kuwa ni kitu ambacho alikuwa akikisubiria kwa muda mrefu. Uamuzi wa kumvua urais wa heshima Milla ulifikiwa juzi katika Mkutano Mkuu wa Fecafoot uliofanyika jijini Younde, uamuzi ambao uliungwa mkono na rais wa shirikisho hilo Mohamed Iya.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment