Tuesday, June 5, 2012

CAMEROON YAMPA LAVAGNE MKATABA WA MWAKA MMOJA.


Denis Lavagne.


KOCHA Denis Lavagne kutoka Ufaransa ambaye amekuwa akiifundisha timu ya taifa ya Cameroon toka Octoba mwaka jana, hatimaye amepewa mkataba wa mwaka mmoja na serikali ya nchi hiyo. Akiongea wakati makabidhiano ya mkataba huo Waziri wa Michezo wa nchi hiyo Adoum Garoua amesema kuwa jukumu kubwa la Lavagne linatakuwa ni kuhakikisha timu hiyo inafanikiwa kufuzu michuano ya Mataifa ya Afrika mwaka 2013 pamoja na ile ya Kombe la Dunia itakayofanyika Brazil 2014. Lavagne ambaye alikuwa kocha wa zamani wa mabingwa wa soka nchini Cameroon klabu ya Coton Sport alichukua mikoba ya kuinoa klabu hiyo kufuatia kutimuliwa kwa aliyekuwa kocha wa timu hiyo Javier Clemente kutoka Hispania baada ya timu hiyo kushindwa kufuzu michuano ya Mataifa ya Afrika iliyochezwa mapema mwaka huu. Mshambuliaji nyota wa zamani wan chi hiyo Roger Millar alikuwa miongoni mwa watu waliopinga uteuzi wa Lavagne kuinoa timu hiyo baada ya kuondoka kwa Clemente na kuunda kamati isiyo rasmi kujaribu kuuondoa uongozi wa Shirikisho la Soka la nchi hiyo ulipo madarakani. Uteuzi huo umekuja ikiwa ni siku mbili baada ya Cameroon kuifunga Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo-DRC kwa bao 1-0 jijini Younde katika mchezo wake wa kwanza wa kutafuta tiketi ya kushiriki michuano ya Kombe la Dunia ambapo inatarajiwa kucheza mchezo mwingine Jumapili dhidi ya Libya.

No comments:

Post a Comment