KLABU ya Celta Vigo imerejea katika Ligi Kuu nchini Hispania baada ya kucheza ligi daraja pili kwa miaka mitano kwa kutoa sare ya bila ya kufungana na klabu ya Cordoba jana na kujihakikishia nafasi ya pili nyuma ya majirani zao klabu ya Deportivo Coruna. Celta Vigo ambao walifikia hatua ya timu 16 bora katika michuano ya Ligi ya Mabingwa mwaka 2004 walikusanya alama 85 katika michezo 42 waliyocheza ikiwa ni alama sita nyuma ya Deportivo ambao walishinda bao 1-0 na kujikusanyia alama 91 kwenye ligi hiyo. Timu za Real Valladolid, Alcorcon, Hercules na Cordoba ambazo zimemaliza katika nafasi ya tatu mpaka sita zitacheza hatua ya mtoano ili kutafuta timu ya mwisho itakayopanda daraja msimu ujao. Kupanda daraja kwa celta Vigo kutaisaidia timu hiyo kupambana na ukata ambao umekuwa ukiwakabili kwa kipindi kirefu sasa baada ya deni lao kufikia kiasi cha euro milioni 51 katika msimu wa 2009-2010. Timu za Racing Santander, Sporting Gijon na Villarreal zimeshuka daraja msimu huu baada ya kumaliza katika tatu za mwisho kwenye ligi kuu nchini humo.
Monday, June 4, 2012
CELTA VIGO YAREJEA LIGI KUU NCHINI HISPANIA BAADA YA MIAKA MITANO.

Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment