Tuesday, July 17, 2012
32 WATEULIWA KUGOMBEA TUZO UEFA.
SHIRIKISHO la Soka barani Ulaya-UEFA limetangaza orodha ya wachezaji 32 ambao wataingia katika mchujo wa kugombani tuzo ya mchezaji bora wa bara hilo. Mabingwa wa Ligi Kuu nchini Hispania inayojulikana kama La Liga klabu ya Real Madrid ndio imetoa wachezaji wengi zaidi katika kinyang’anyiro cha tuzo hizo wakiwa na wachezaji saba wakifuatiwa na mabingwa wa Ligi Kuu nchini Uingereza, Manchester City iliyotoa wachezaji sita. Mabingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, Chelsea na Barcelona kila timu imetoa wachezaji wanne wakati Radamel Falcao ndiye mchezaji pekee kutoka kwa mabingwa wa Ligi ya Ulaya maarufu kama Europa League klabu ya Atletico Madrid kuingia katika orodha hiyo. Wachezaji hao wamechaguliwa na jopo la waandishi wa habari kutoka vyama 53 ambavyo ni wajumbe wa UEFA ambapo katika mchujo yatabakia majina matatu ambayo yatapata kura nyingi zaidi za waandishi kabla ya mshindi kutangazwa jijini Monaco, Ufaransa Agosti 14 mwaka huu. Katika tuzo zilizopita mshambuliaji nyota wa Barcelona Lionel Messi ndiyo alinyakuwa tuzo hiyo akiwashinda Xavi Hernandez ambaye wanacheza timu noja na Cristiano Ronaldo wa Real Madrid.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment