Sunday, July 8, 2012

ADVOCAAT AMKINGIA KIFUA VAN GAAL.

Dick Advocaat.

KOCHA Dick Advocaat ambaye ni raia wa Uholanzi amekubaliana na uamuzi wa Chama cha Soka cha nchi hiyo-KNVB kumteua Louis van Gaal kuwa kocha mpya wa kikosi hicho akisisitiza kocha huyo ni mtu sahihi kwa kazi hiyo. Van Gaal aliiwezesha Ajax Amsterdam kunyakuwa taji la michuano ya Klabu ya Ulaya mwaka 1995 na amewahi kushinda mataji ya ligi katika nchi za Hispania na Ujerumani wakati akizinoa klabu za Barcelona na Bayern Munich. Pamoja na kutimuliwa kwa kocha huyo miaka 10 iliyopita kukinoa kikosi cha Uholanzi baada ya kushindwa kuipeleka timu kwenye michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2002, Advocaat amemfagilia Van Gaal kwamba kutokana na mafanikio aliyopata mpaka sasa anastahili kupewa nafasi nyingine. Advocaat ambaye kwasasa ni kocha wa klabu ya PSV aliendelea kusema kuwa hakuna taji ambalo Van Gaal hajashinda hivyo kumfanya kuwa kocha wa kiwango cha juu kwasasa ambapo kwa uwezo wake huo anaweza kuipeleka mbali Uholanzi. Van Gaal ambaye amenyakuwa mataji matatu ya ligi nchini Uholanzi wakati anafundisha klabu ya Ajax anatarajiwa kuasaidiwa na nahodha wa zamani Danny Blind.

No comments:

Post a Comment