BOLT, BLAKE FITI KWA OLIMPIKI - DAKTARI.
 |
Usain Bolt. |
DAKTARI wa wanariadha nyota wa mbio fupi, Usain Bolt na Yohan Blake kutoka Jamaica, Winston Dawes amesema kuwa wanariadha hao wako katika hali nzuri kiafya tayari kwa ajili ya michuano ya olimpiki inayotarajiwa kuzinduliwa rasmi kesho. Dawes aliwaondoa hofu mashabiki wa mbio hizo kwamba Bolt angekosa michuano hiyo kutokana na kuwa majeruhi na kuwa ahidi wategemee makubwa kutoka kwa wanariadha hao ambao wananolewa na kocha mmoja. Bolt ambaye ni bingwa mtetezi wa mbio za mita 100 na 200 katika michuano hiyo alikuwa akisumbuliwa na maumivu ya mgongo lakini Dawes amesema kuwa kwasasa yuko vyema na hana maumivu hayo yaliyokuwa yakimkabili tena. Bolt ndiye anayeshikilia rekodi za dunia za sekunde 9.58 katika mbio za mita 100 na sekunde 19.19 katika mbio za mita 200 lakini Blake alimshinda Bolt katika umbali huo wote katika mbio za majaribio zilizofanyika nchini Jamaica mwezi mmoja uliopita.
No comments:
Post a Comment