Thursday, July 19, 2012

CHELSEA YAENDELEZA UBABE MAREKANI.

KLABU ya Chelsea ya Uingereza jana imefanikiwa kushinda mabao 4-2 dhidi ya timu ya Seatlle Sounders katika mchezo wa kirafiki uliofanyika nchini Marekani ambapo timu hiyo iko katika ziara kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa Ligi Kuu ya Uingereza. Mabao ya Chelsea ambao huo unakuwa ni mchezo wao wa kwanza toka wanyakue taji la michuano ya Klabu Bingwa Ulaya kwa kuifunga Bayern Munich katika mchezo wa fainali, yalifungwa na mshambuliaji wake kinda kutoka Ubelgiji Romelu Lukaku ambaye alifunga mawili katika kipindi cha kwanza. Wakati mabao mengine yalifungwa katika kipindi cha pili na mshambuliaji mpya ambaye amesajili msimu huu wa klabu hiyo Eden Hazard na Marko Marin ambao kila mmoja alifunga bao moja. Mabao ya Seattle yalifungwa na Fredy Montero katika kipindi cha kwanza lakini timu hiyo itabidi ijilaumu kwa kushindwa kufunga mabao zaidi kutokana na kukosa nafasi nyingi za wazi walizopata.

No comments:

Post a Comment