Tuesday, July 10, 2012

FIFA YAIUNGA MKONO FKF KWA KUWASIMAMISHA VIONGOZI WA SOKA.

Add caption

SHIRIKISHO la Soka la Dunia-FIFA limekubaliana na uamuzi ulichukuliwa na Shirikisho la Soka nchini Kenya-FKF la kuwasimamisha makamu mwenyekiti Sammy Sholei na mwenyekiti wa tawi la Nairobi Dan Shikanda. Viongozi hao wawili walitimuliwa wiki iliyopita baada ya kulifikisha shirikisho la nchi hiyo mahakamani wakipinga suala la upitishwaji wa katiba mpya ya FKF. FIFA kupitia Katibu mkuu wake Jerome Valcke alithibitisha kupokea barua hiyo ambayo kamati ya utendaji ya FKF imechukua jukumu la kuwasimamisha viongozi hao wawili kujishughulisha na masuala yoyote ya soka mpaka hapo shauri lao litakaposikilizwa na kutolewa maamuzi. Valcke amesema kuwa kamati hiyo ina haki hiyo kikatiba lakini suala hilo linatakiwa kupelekwa katika mkutano mkuu unaokuja wa FKF ambapo watuhumiwa wataruhusiwa kujitetea wenyewe kuhusiana na suala hilo.

No comments:

Post a Comment