HALI YA EUSEBIO YATENGEMAA.
 |
Eusebio. |
NGULI wa zamani wa soka wa Ureno na klabu ya Benfica, Eusebio da Silva Ferreira anaendelea vizuri na matibabu baada ya nyota huyo kupata mshtuko wa moyo. Eusebio ambaye ana umri wa miaka 70 amelazwa katika hospitali iliyopo jijini Lisbon akiendelea na matibabu toka alipougua wakati wa michuano ya Ulaya mwezi uliopita. Benfica wamesema kuwa nyota wao huyo wa zamani bado ataendelea kupatiwa matibabu na anaweza kuruhusiwa kurejea nyumbani mwishoni mwa wiki hii kama hali yake ikiendelea kutengemaa. Hiyo ni mara ya nne kwa Euesebio kulazwa toka Desemba mwaka jana kutokana na maradhi mbalimbali yanayomsumbua. Eusebio amekuwa nyota wa Ureno ambaye hawezi kusaulika kutokana na kiwango cha hali ya juu alichokionyesha katika kipindi ccha miaka ya 1960 na Shirikisho la Soka la Dunia-FIFA walimtaja kama mmoja wa wachezaji 10 bora waliowahi kucheza soka tuzo iliyotolewa mwaka 1998.
No comments:
Post a Comment