Wednesday, July 25, 2012

OLIMPIKI 2012: SENEGAL KUFUNGUA NA WENYEJI, MISRI USO KWA USO NA BRAZIL.

Nahodha wa Misri, Mohamed Abutrika.
 TIMU ya Taifa ya Misri inatarajiwa kutupa karata ya kwanza kesho kwenye michuano ya Olimpiki wakati itakapomenyana na Brazil katika mchezo utakaofanyika katika Uwanja wa Millenium uliopo jijini Cardiff, Wales. Hiyo itakuwa ni mara ya kwanza kwa nchi hiyo kushiriki michuano hiyo toka mwaka 1992 ambapo tumeshuhudia katika siku za karibuni imekumbwa na matatizo ya kisiasa baada ya kiongozi wake wa zamani Hosni Mubaraka kuondoka madarakani kwa shinikizo la wandamanaji na kuchaguliwa kiongozi mpya Mohamedi Morsi kwa njia ya demokrasia. Kikosi cha Misri kitaingia uwanjani kujaribu kunyakuwa medali ya dhahabu kwenye michuano hiyo ili kuonyesha ulimwengu kuwa bado wamo kwenye soka, baada ya Ligi Kuu nchini humo kufutwa kutokana na vurugu zilizosababisha vifo vya watu zaidi ya 70 na kujeruhi mamia wengine. Mbali na Misri timu zingine ambazo zitaliwakilisha bara la Afrika kesho na nchi watakazocheza nazo ni Gabon itacheza na Switzerland, Morocco itachuana na Honduras huku Senegal wakifungua michuano hiyo na mwenyeji Uingereza.

No comments:

Post a Comment