Monday, July 23, 2012

RAIS WA SOKA LIBYA AJIUZULU.

Kuweidir Muftah.
RAIS wa Shirikisho la Soka nchini Libya, Kuweidir Muftah amejiuzulu wadhfa wake huo baada ya kukemewa na kupata shinikizo kutoka mamlaka. Akihojiwa kuhusiana na taarifa hizo Muftah alithibisha kuachia ngazi katika shirikisho hilo akidai kuwa amekuwa akipata shinikizo lakufanya hivyo kutokana na mwenendo usioridhisha wa shirikisho hilo. Kujiuzulu kwa Maftah kumekuja ikiwa siku chache toka Mwenyekiti wa Kamati ya Olimpiki wa nchi hiyo, Ahmed Nabil al-Taher al-Alam kutekwa jijini Tripoli na watu wasiojulikana ambao walijifanya kama maofisa polisi. Taher al-Alam aliachiwa bila kujeruhiwa Jumapili katika mji wa Misrata ambapo majeshi ya waasi yalimsaidia kumrudisha katika mji mkuu wakishirikiana na maofisa wa usalama kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na serikali ya nchi hiyo. Ujumbe wa olimpiki uliondoka nchini humo Jumamosi kuelekea London, Uingereza ambapo ujumbe huo umejumuisha wanariadha watano ambao wanatarajiwa kushiriki katika michuano hiyo.

No comments:

Post a Comment