NAHODHA wa zamani wa timu ya taifa ya Uingereza, John Terry amekutwa hana hatia kutokana na tuhuma za kibaguzi alizomfanyia mchezaji mwenzake Anton Ferdinand baada ya siku tano za usikilizwaji wa kesi hiyo. Terry mwenye miaka 31, ambaye anapokea kitita cha paundi 150,000 kwa wiki akiwa kama nahodha wa klabu ya Chelsea alikuwepo katika mahakama ya Westminster mbele hakimu Howard Riddle akisikiliza hukumu hiyo. Kesi hiyo ya kutoleana maneno makali baina ya wachezaji hao wawili wakati wa mchezo wa Ligi Kuu nchini Uingereza Oktoba mwaka jana ilisababisha aliyekuwa kocha mkuu wa timu ya taifa ya nchi hiyo Fabio Capello kujiuzulu kufuatia Chama cha Soka cha nchi hiyo kumvua unahodha Terry. Terry alikana tuhuma za ubaguzi dhidi ya Ferdinand ingawa katika utetezi wake alikiri kuwa alitumia maneno makali wakati wakijibishana kwenye mchezo huo. Terry amesema kuwa alichukizwa na kitendo cha mchezaji huyo kujiangusha na kutaka penati wakati wa mchezo baina ya timu zao.

Saturday, July 14, 2012
TERRY HANA HATIA.

Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment