VAN PERSIE ATAKA KULIPWA PAUNDI 195,000.
 |
| Robin van Persie. |
MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Uholanzi na klabu ya Arsenal, Robin van Persie amebainisha kuwa anahitaji kulipwa kiasi cha paundi milioni 10 mwaka kama kuna timu yoyote itahitaji saini yake katika kipindi hiki cha majira ya kiangazi. Wakala wa mchezaji huyo Kees Vos alikutana na mabingwa wa Ligi Kuu ya soka nchini Italia klabu ya Juventus na kubainisha kuwa mteja wake huyo anahitaji kulipwa mshahara unaofikia kiasi cha paundi 195,000 kwa wiki. Kama klabu zinazomuwania zikikubali kumlipa kiasi hicho kitamfanya van Persie awe mmoja ya wachezaji wanaolipwa zaidi duniani katika mchezo wa soka. Mbali ya Juventus kumhitaji mchezaji huyo pia Manchester United na Manchester City nazo zimeingia katika mbio za kumuwania mchezaji huyo ambaye ana umri wa miaka 28. Van Persie ambaye amewahi kushinda mara mbili taji la mchezaji bora wa mwaka nchini Uingereza tayari amekataa mshahara wa paundi 130,000 kwa wiki atakazopewa na Arsenal lakini hakuna klabu yoyote kati ya United au City walioogopa kumlipa kiasi hicho. City inamlipa kiungo wa kimataifa wa Ivory Coast Yaya Toure paundi 225,000 kwa wiki wakati Wayne Rooney anapokea kiasi cha paundi 200,000 kutoka kwa United.
No comments:
Post a Comment