Monday, August 6, 2012

AFC YAMSHIKIA BANGO BIN HAMMAM.

Shirikisho la Soka barani Asia limewataka nchi wanachama 46 wa shirikisho hilo kutoa ushirikiano kutokana na uchunguzi dhidi ya tuhuma za rushwa zinaomkabili rais wa shirikisho hiolo aliyesimamishwa Mohamed bin Hammam. Katika taarifa iliyotolewa na Zhang Jilong ambaye ndiye anakaimu nafasi ya Bin Hammam amesema katika taarifa yake kuwa Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho hilo imeomba uongozi kumuajiri mkurugenzi wa zamani wa FBI, Louis Freeh kusaidia katika uchunguzi huo. Bin Hammam anatuhumiwa kujitajirisha mwenyewe na kuchota mamilioni ya dola katika kipindi cha miaka tisa ambayo amekuwa kiongozi wa shirikisho hilo. Freeh ndio aliyekuwa kiongozi wa uchunguzi wa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA dhidi ya Bin Hammam kutokana na tuhuma za kujaribu kuwahonga wapiga kura wakati wa kipindi cha kampeni za uchaguzi dhidi ya Sepp Blatter ambaye alishinda uchaguzi huo. Matokeo ya uchunguzi huo yalipelekea Bin Hammam kufungiwa maisha kujishughulisha na masuala ya soka mwaka jana lakini adhabu hiyo ilitenguliwa mwezi uliopita na Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo kwa madai kuwa hakukuwa na ushahidi wa kutosha.

No comments:

Post a Comment