Monday, August 20, 2012
AFC YAMUONGEZA BIN HAMMAM KIFUNGO CHA SIKU 20 ZAIDI.
SHIRIKISHO la Soka barani Asia-AFC limeongeza siku 20 za uchunguzi dhidi rais wa zamani wa shirikisho hilo Mohamed bin Hammam juu ya tuhuma za matumamizi mabaya ya fedha wakati akiwa madarakani. Bin Hammam ambaye ni raia wa Qatar alifungiwa kwa siku 30 lakini mwenyeti wa Kamati ya Nidhamu wa AFC, Lim Kia Tong aliongeza adhabu hiyo ikiwa ni siku moja ilikuwa imebakia adhabu yake ya mwanzo kuisha. Bin Hammam pia anachunguzwa tena na Shrikisho la Soka la Dunia-FIFA ambao walimfungia maisha kutokana na makosa ya kutoa rushwa lakini alikata rufani na kushinda katika Mahakama ya Usuluhishi ya Michezo-CAS mwezi uliopita. Bin Hammam ambaye ana umri wa miaka 63 alichaguliwa kwa kipindi cha tatu mfululizo katika uchaguzi wa AFC Januari mwaka jana kabla ya kuamua kugombea nafasi ya urais wa FIFA dhidi ya Sepp Blatter mwezi mmoja baadae. Bin Hammam alijitoa katika kinyang’anyiro hicho baada ya kukabiliwa na tuhuma za kuwahonga ili wampigie kura viongozi wa soka wa Caribbean kwa kuwapa kila mmoja dola 40,000 wakati alipokutana na viongozi hao nchini Hispania.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment