Tuesday, August 14, 2012

BIN HAMMAM KUPAMBANA NA FIFA NA AFC.

ALIYEWAHI kuwa mgombea urais wa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA, Mohamed bin Hammam amesema kuwa atachukua hatua kwa shirikisho hilo kumfungia tena kwa siku 90 baada ya Mahakama ya Usuluhishi ya Michezo-CAS kumuachia kutengua adhabu yake ya kufungiwa maisha kujishughulisha na masuala ya michezo. FIFA ilimfungia maisha Bin Hammam baada ya kumkuta na hatia ya kujaribu kununua kura kutoka kwa maofisa wa Caribbean katika uchaguzi uliofanyika mwaka jana lakini CAS ilimwachia huru kutokana na kukosekana kwa ushahidi wa kutosha ili kumtia hatiani Bin Hammam. Mbali na kufungiwa na FIFA Bin Hammam ambaye pia ni rais wa Shirikisho la Soka barani Asia-AFC amefungiwa na shirikisho hilo kwa siku 30 ili kupisha uchunguzi juu ya tuhuma zingine za matumizi mabaya ya ofisi. Bin Hammam amesema kuwa timu ya wanasheria yake inajiandaa kuchukua hatua ya kile anachodai uonevu anafanyiwa na FIFA ambapo atatangaza hatua atazochukua hapo baadae watapokamilisha utetezi wao.

No comments:

Post a Comment