Thursday, August 2, 2012

CARLOS ATUNDIKA DALUGA.

Roberto Carlos.
BEKI wa klabu ya Anzhi Makhachkala ya Urusi, Roberto Carlos ametangaza kustaafu rasmi mchezo wa soka likiwa ni tukio la ghafla baada ya kipindi cha nyuma kusema kuwa anaweza kuendelea kucheza kwa muda mwingine zaidi. Carlos mwenye miaka 39 amekuwa akifanya kubwa ya kuitangaza Anzhi katika miezi ya karibuni na anatarajiwa kuwa kocha msaidizi wa klabu hiyo tajiri mara atakapopata leseni yake ya ukocha. Beki huyo mahiri alihamia klabu ya Inter Milan ya Italia mwaka 1995 baada ya kuichezea kwa miaka miwili klabu ya Palmeiras lakini alidumu klabuni hapo kwa msimu mmoja kabla ya kusajiliwa na Real Madrid. Akiwa Santiago Bernabeu nyota huyo wa kimataifa wa Brazil aliisaidia klabu hiyo kushinda mataji manne ya Ligi Kuu nchini Hispania maarufu kama La Liga, mataji matatu ya Ligi ya Mabingwa Ulaya na mataji matatu ya Kombe la Mfalme. Baada ya miaka 11akiwa Madrid Carlos alihamia klabu ya Fernabahce ambayo aliichezea kwa miaka miwili kabla ya kwenda Corinthians na baadae Anzhi ambayo alijiunga nayo mwaka jana. Amecheza michezo 125 akiwa na timu ya taifa ya Brazil na alikuwa sehemu ya kikosi cha nchi hiyo ambacho kilinyakuwa taji la Kombe la Dunia mwaka 2002 na Copa America mwaka 1997 na 1999.

No comments:

Post a Comment