Wednesday, August 15, 2012

MISRI KUJIPIMA NGUVU NA SAUDI ARABIA.

KOCHA msaidizi wa timu ya taifa ya Misri, Diaa Al Sayed amebainisha kuwa timu hiyo inatarajiwa kucheza mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Saudi Arabia Septemba mwaka huu jijini London, Uingereza. Al Sayed amesema kuwa Chama cha soka cha nchi hiyo kimepokea maombi matatu ya michezo ya kirafiki kutoka kwa Saudi Arabia, Uruguay na China na wamekubali kucheza na Saudi Arabia lakini pia bado wanapitia maombi mengine na watazungumza na wadhamini wao waone kama kuna uwezekano wa kucheza michezo hiyo. Kocha huyo aliendelea kusema kuwa kwasasa timu hiyo haina mechi ya mashindano mpaka Machi mwakani hivyo itakuwa vyema kwao kucheza michezo ya kirafiki ili kuwaweka vyema wachezaji wa timu hiyo. Misri ambao wameenguliwa katika michuano ya Mataifa ya Afrika na jamhuri ya Afrika ya Kati Mei mwaka huu, wanatarajia kucheza mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Oman baadae leo.

No comments:

Post a Comment