Friday, September 7, 2012

ESPERANCE KLABU BORA AFRIKA.

SHIRIKISHO la Kimataifa la Historia na Takwimu katika mchezo wa Soka-IFFHS, ambao wanashughulika na historia na kumbukumbu ya vyama vya soka wametoa orodha ya klabu bora 400 duniani za soka. Klabu ya Barcelona ya Hispania imeendelea kubakia katika nafasi yake ya kwanza wakiwa wamejikusanyia alama 346 wakati klabu ya CD Universidad de Chile Santiago ya Chile ikishika nafasi ya pili kwakuwa na alama 317 wakifuatiwa na Real Madrid ambao wana alama 293. Mabingwa wa Ligi ya Mabingwa Afrika, Esperance ya Tunisia ndio inayoongoza katika orodha ya klabu bora Afrika wakiwa katika nafasi ya 61 duniani baada ya kupanda nafasi 10 kutoka nafasi ya 71 katika orodha zilizopita. Timu nyingine 10 kutoka Afrika zilizoshika nafasi za juu katika orodha hiyo ni pamoja na Al Hilal Omdurman ya Sudan ambayo iko katika nafasi ya 82 wakiwa na alama 127, Sunshine Stars ya Nigeria nafasi ya 140 wakiwa na alama 104, Al Merreikh Omdurman ya Sudan nafasi ya 146 wakiwa na alama 103 na MAS Fes ya Morocco nafasi ya 149 wakiwa na alama 102. Nyingine ni Al Ahly ya Misri nafasi ya 151 wakiwa alama 102, Zamalek ya Misri nafasi ya 151 wakiwa na alama 102, Grupo Desportivo Interclube Luanda ya Angola nafasi ya 160 wakiwa na alama 99, Chelsea FC Berekum ya Ghana nafasi ya 171 wakiwa na alama 96 na kumi bora inafungwa na Enyimba International FC ya Nigeria nafasi ya 229 wakiwa na alama 83.

No comments:

Post a Comment