Saturday, September 8, 2012

FIFA KUMJADILI PARK.

SHIRIKISHO la Soka Duniani-FIFA limesema kuwa mchezaji wa kimataifa wa Korea Kusini ambaye alionyesha alama inayohusiana na masuala ya kisiasa wakati akipokea medali ya shaba katika michuano ya Olimpiki iliyofanyika London mwaka huu, anatarajiwa kujadiliwa na kamati ya nidhamu ya shirikisho hilo Octoba 5 mwaka huu. Kamati hiyo itasaidia kuamua kama mchezaji huyo anayeitwa Park Jong-woo apewe medali yake ambayo Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki-IOC iliizuia toka Agosti 10 kutokana na tukio hilo. Baada ya Korea Kusini kufanikiwa kuifunga Japan kwa mabao 2-0 katika Uwanja wa Cardiff, mchezaji huyo alionyesha alama ya kukishabikia chama kimoja cha siasa nchini kwake kitendo ambapo kililalamikiwa pia na Japan. IOC na FIFA ilipiga marufuku wachezaji kuonyesha alama au maneno ambayo yanahusiana na masuala ya siasa pindi wawapo uwanjani. IOC iliiagiza Kamati ya Olimpiki ya Korea Kusini kuhakikisha Park hapokei medali yake katika Uwanja wa Wembley siku mbili baada ya kufanya tukio hilo.

No comments:

Post a Comment