Wednesday, September 12, 2012

MURRAY ATAMANI MATAJI ZAIDI YA GRAND SLAM.

BINGWA wa michuano ya tenisi ya wazi ya Marekani maarufu kama US Open, Andy Murray amesema kuwa lengo lake kubwa ni kushinda mataji mengi zaidi ya Grand Slam na kuwa mchezaji namba moja katika orodha za ubora duniani. Murray ambaye kwasasa anashika namba tatu katika orodha hizo amesema kuwa kwa kiwango alichofikia hivi sasa anaamini kuwa naweza kufikia ndoto zake hizo za kuwa mchezaji bora kabisa wa mchezo huo. Nyota huyo aliendelea kusema kuwa ili kufikia ndoto hizo hizo anahitaji kucheza kwa kiwango cha juu zaidi kitu ambacho nyota wenzake kama Novak Djokovic, Roger Federer na Rafa Nadal wamekuwa wakifanya vizuri. Baada ya kukata kiu ya miaka 76 na kuwa mwingereza wa kwanza kushinda taji la Grand Slam, Murray amepania kuendelea kuweka historia zaidi na kushinda taji la Wimbledon.

No comments:

Post a Comment