Monday, September 3, 2012

US OPEN: AZARENKA KUKWAANA NA BINGWA MTETEZI SAM STOUR KATIKA ROBO FAINALI.

MCHEZAJI tenisi anayeongoza katika orodha za ubora duniani kwa upande wa wanawake, Victoria Azarenka amefanikiwa kutinga katika hatua ya robo fainali kwa mara ya kwanza katika michuano ya wazi ya Marekani baada ya kumfunga Anna Tatishvili. Katika mchezo huo Azarenka alitumia muda wa dakika 82 kumsambaratisha Tatishvili kwa 6-2 6-2 ambapo sasa atakutana na bingwa mtetezi wa michuano hiyo Sam Stour kwenye hatua ya robo fainali. Maria Sharapova ambaye anashika namba tatu katika michuano hiyo naye alifanikiwa kutinga katika hatua ya robo fainali ya michuano hiyo baada ya kumuondosha Nadia Petrova 6-1 4-6 6-4. Sharapova atakutana na Mario Bartoli wa Ufaransa baada ya mchezaji huyo kumuondosha Petra Kvitova kwa 1-6 6-2 6-2. Kwa upande wa wanaume bingwa mtetezi wa michuano hiyo Novac Djokovic amefanikiwa kusonga mbele baada ya kumfunga kirahisi Julien Benneteau wa Ufaransa kwa 6-3 6-2 6-2 katika mzunguko wa tatu. Nyota mwingine wa mchezo huo Andy Roddick ambaye ametangaza kustaafu baada ya michuano hiyo amefanikiwa kumfunga Fabio Fognini ambapo sasa anatarajiwa kukutana na Juan Martin del Porto ambaye ni bingwa wa michuano hiyo mwaka 2009.

No comments:

Post a Comment