Thursday, October 4, 2012

BLANC ANENA KUWA WAAJIRI WAKE WALIKUWA HAWAMTAKI.

ALIYEKUWA kocha wa timu ya taifa ya Ufaransa, Laurent Blanc amebainisha kuwa alijiengua katika nafasi hiyo kwasababu Shirikisho la Soka la Ufaransa lilikataa kumuongeza mkataba mwingine. Blanc aliacha kukinoa kikosi cha nchi hiyo baada ya kupoteza mchezo dhidi ya waliokuja kuwa mabingwa wa michuano ya Ulaya 2012 Hispania kwa mabao 2-0 katika mchezo wa robo fainali. Akihojiwa kocha huyo ambaye naye pia amewahi kucheza katika kikosi cha nchi hiyo amesema kuwa alikuwa akisubiri waajiri wake wamuongeze mkataba mwingine lakini walionekana kukaa kimya hivyo akaona bora aondoke mwenyewe kwa kuwa hawakuonekana kumuhitaji. Blanc alifafanua kuwa kuondoka kwake hakukutokana na wachezaji ambao baada ya michuano ya hiyo waliitwa na Kamati ya Nidhamu ya shirikisho hilo kutokana na tabia za utovu wa nidhamu walizozionyesha. Wachezaji ambao waliitwa na kamati hiyo ni pamoja na Samir Nasri, Jeremy Menez, Yann M’Vila na Hatem Ben Arfa ambapo kati ya hao Nasri alifungiwa michezo mitatu na Menez mchezo mmoja.

No comments:

Post a Comment