Sunday, October 7, 2012

FA KUCHUNGUZA TUHUMA ZA UBAGUZI DHIDI YA WACHEZAJI WA BOLTON.

Chama cha Soka nchini Uingereza-FA kinachunguza tuhuma za ubaguzi wa rangi zilizotolewa na mchezaji wa Bolton Wanderers MARVIN SORDELL wakati timu hiyo ilipofungwa na timu ya Millwall. SORDELL mwenye umri wa miaka 21 aliandika katika mtandao wake wa kijamii wa twitter kuwa mbali nay eye kushambuliwa kwa maneno ya kibaguzi lakini pia yaliwalenga wachezaji wenzake LEE CHUNG-YONG, DARREN PRATLEY na BENIK AFOBE. Klabu hizo mbili pia zinachunguza tuhuma hizo zilizotolewa na Sordell ambaye anadai alisikia maneno hayo wakati anapasha misuli ili aweze kuingia katika mchezo huo wa Ligi Daraja la Kwanza uliofanyika katika Uwanja wa The Den Jana. Msemaji wa Bolton amesema kuwa klabu hiyo kwa kushirikiana na Millwall watalifanyia uchunguzi tukio hilo kwa pamoja na wanatarajia kuzungumza maaskari waliokuwepo uwanjani pamoja na waamuzi wa mchezo huo.

No comments:

Post a Comment