FA YATOA TAARIFA HUKUMU YA TERRY.
|
Ferdinand na Terry. |
CHAMA cha soka cha Uingereza-FA kimetoa taarifa kuelezea kwanini walikataa utetezi wa nahodha wa klabu ya Chelsea John Terry na kumkuta na hatia ya kumfanyia vitendo vya kibaguzi mlinzi wa Queens Park Rangers Antony Ferdinand msimu uliopita. FA ilitoa taarifa hiyo yenye kurasa 63 kuelezea sababu za kumfungia mechi nne na kumtoza faini ya paundi 220,000 kutokana na tukio hilo ambalo lilitokea wakati wa mchezo wa Ligi Kuu nchini Uingereza uliochezwa katika Uwanja wa Loftus Road. Terry ambaye amepewa mpaka Octoba 18 awe amekata rufani, mwezi Julai mwaka huu mahakama ya jijini London ilimkuta hana hatia kuhusiana na tukio hilo. Katika utetezi wake Terry alikiri kutumia neon black likimaanisha mtu mweusi wakati walipokwaruzana na beki huyo ambaye ni ndugu na Rio Ferdinand wa Manchester United.
No comments:
Post a Comment