Wednesday, November 14, 2012
WANYAMA KUIKOSA TAIFA STARS.
KIUNGO wa kimataifa wa Kenya, Victor Wanyama anaendelea vizuri na matibabu ya koo baada ya kupata maambukizi. Akihojiwa na mtandao wa Supersport Wanyama amesema kuwa kwasasa yuko chini ya uangalizi wa madaktari na anatarajia kurejea mazoezini kati ya Ijumaa au Jumatano wiki ijayo. Wanyama pia alitumia nafasi hiyo kuitakia ushindi timu yake ya taifa ya Kenya Harambe Stars ambayo itakuwa na kibarua kigumu cha kupambana na timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars katika Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza. Wanyama alikumbwa na tatizo hilo baada ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya baina ya klabu yake ya Celtic na Barcelona mchezo ambao walishinda kwa mabao 2-1 huku bao moja akifunga Wanyama. Kuhusu taarifa za yeye kuhamia katika klabu ya Manchester United katika kipindi cha dirisha dogo Wanyama amesema kuwa hata mwenyewe anasikia taarifa kama hizo hivyo itajulikana kikifika kipindi hicho lakini kwasasa anaelekeza nguvu zake kuisaidia Celtic kadri awezavyo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment