Monday, December 17, 2012

BRAZIL YAZINDUA UWANJA WA KWANZA UTAKAOTUMIKA KWA AJILI YA KOMBE LA DUNIA.

UWANJA wa Castelao Arena uliopo kaskazini-mashariki mwa Brazil katika mji wa Fortaleza umekuwa uwanja wa kwanza kukamilika kwa ajili ya michuano ya Kombe la Dunia inayotarajiwa kufanyika nchini humo mwaka 2014. Sambamba na Uwanja wa Mineirao uliopo jijini Belo Horizonte ambao utafunguliwa Desemba 21 ndivyo vinakuwa viwanja pekee kukamilika kwa wakati kabla ya michuano ya Kombe la shirikisho itakayochezwa Juni mwakani. Rais wan chi hiyo Dilma Rousseff alihudhuria sherehe za ufunguzi wa uwanja wa Castelao ambao umekamilika kwa kutumia gharama za dola milioni 249 ukiwa na uwezo wa kuingiza mashabiki 67,000. Rousseff amesema kuwa kukamilika kwa uwanja huo kwa ajili ya michuano ya 2014 na ushindi wa timu ya Corinthians katika michuano ya Kombe la Klabu Bingwa ya Dunia jana unaonyesha jinsi gani Brazil ilivyokuwa na uwezo ndani na nje ya uwanja. Amesema nchi hiyo inauwezo wa kufanya vyote viwili kushinda mataji uwanjani na kujenga uwanja bora kama huo uliofunguliwa jana.

No comments:

Post a Comment