Wednesday, December 26, 2012

ROONEY NJE WIKI MBILI.

MSHAMBULIAJI wa Manchester United, Wayne Rooney anatarajiwa kukaa nje ya uwanja wa kipindi cha wiki mbili hadi nne baada ya kuumia mguu wakati wa mazoezi ya timu hiyo kabla ya mchezo wa jana wa Ligi Kuu nchini Uingereza dhidi ya Newcastle United. Rooney hakuwemo katika kikosi kilichoanza katika mchezo ambao walishinda mabao 4-3 dhidi ya Newcastle katika Uwanja wa old Trafford na meneja wa klabu hiyo Sir Alex Ferguson amesema kuwa mshambuliaji huyo atakosa michezo yote kwa mwaka huu. Kocha huyo aliiambia tovuti ya klabu hiyo kuwa nyota huyo aliumia dakika za mwisho mazoezini wakati akijaribu kuruka juu ndipo alipojiumiza kifundo cha mguu wake wa kulia. United inakabiliwa na mchezo dhidi ya West Bromwich Albion Jumamosi kabla ya kusafiri kufuata Wigan Athletic Januari Mosi ambapo wanajipanga kujizatiti kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo.

No comments:

Post a Comment