Saturday, January 5, 2013

AGUERO ATENGANA NA MTOTO WA MARADONA.

MSHAMBULIAJI nyota wa kimataifa wa Argentina na klabu ya Manchester City, Sergio Aguero ametengana na mkewe Giannina ambaye ni mtoto wa Diego Maradona baada ya doa hiyo kudumu kwa miaka minne. Giannina kwasasa inaaminika kuwa anaishi jijini Madrid, Hispania pamoja na mtoto wao wa kiume mwenye miaka mitatu baada ya kuthibitisha taarifa hizo katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter. Giannina aliandika katika mtandao kuwa wametengana na mumewe kabla ya kuongeza kuwa ulikuwa mwaka mgumu na kulikuwa na mambo mengi yaliyobadilika. Katika mtandao mmoja wa mashabiki alimjibu Giannina kuwa Aguero hakustahili kuwa naye kwani ni mjinga na mpumbavu lakini mwanamama alimtetea mumewe huyo na kumwambia mshabiki huyo asiseme hivyo kwa baba wa mtoto wake kwani hafanani na maneno anayosema.

No comments:

Post a Comment