Thursday, January 17, 2013
AUSTRALIA OPEN: SHARAPOVA, VENUS KUKWAANA.
WACHEZAJI tenisi nyota Maria Sharapova wa Urusi na Venus Williams wa Marekani wanatarajia kukwaana katika mzunguko wa tatu wa michuano ya wazi ya Australia inayoendelea jijini Melbourne. Venus anatarajia kutumia ushauri atakaopewa na dada yake Serena ambaye amewahi kumfunga Sharapova anayeshika namba mbili katika orodha za ubora dunia, mara zote tisa walizokutana katika mashindano mbalimbali. Serena amesema yuko tayari kumsaidia dada yake huyo ambaye kwa kipindi kirefu amekuwa nje uwanja kutokana na majeruhi na baadae kuumwa ili aweze kushinda mchezo huo unaotarajiwa kuwa na mkali na wa kusisimua. Mwanadada huyo ambaye anapewa nafasi kubwa ya kutwaa taji la michuano hiyo amesema utakuwa mchezo mkubwa na anadhani dada yake Venus ambaye hajashinda taji lolote toka mwaka 2008 hana cha kupoteza katika mchezo huo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment