Sunday, January 20, 2013
ILIKUWA LAZIMA TUFUNGWE KWA NAMNA MOJA AU NYINGINE - MESSI.
MSHAMBULIAJI nyota wa klabu ya Barcelona, Lionel Messi amesema kufungwa mabao 3-2 na Real Sociedad Jumamosi ni kitu ambacho hakijawashangaza sana, lakini aliongeza kuwa inabidi wasahau suala hilo na kuhakikisha wanashinda mchezo wa Kombe la Mfalme katikati ya wiki ijayo. Pamoja na kuifungia bao timu yake katika mechi 10 mfululizo kwenye Ligi Kuu nchini Hispania maarufu kama La Liga, Siciedad hawakukata tama baada ya kutoka nyuma na kuhakikisha wanaondoka na alama zote tatu. Akihojiwa mara baada ya mchezo huo Messi ambaye ni mshindi wa tuzo ya Ballon d’Or amesema kupoteza mchezo ni kitu ambacho kilitegemewa na kitu cha muhimu hivi sasa ni kusahau hilo na kuzingatia mchezo unaofuata. Barcelona ambao walicheza pungufu katika mchezo huo baada ya beki wake Gerard Pique kupewa kadi ya pili ya njano na kutolewa nje inatarajia kusafiri kuifuata Malaga Jumatano katika mchezo wa robo fainali ya Kombe la Mfalme.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment