Monday, January 14, 2013

KOMPANY ATETEA RAFU YAKE.

NAHODHA wa klabu ya Manchester City, Vincent Kompany ametetea rafu aliyocheza ambayo ilipelekea kutolewa nje kwa kadi nyekundu katika mchezo walioshinda mabao 2-0 dhidi ya Arsenal katika Uwanja wa Emirates. Kompany mwenye umri wa miaka 26 alitolewa nje na mwamuzi Mike Dean kwa faulo ya hatari aliyocheza dhidi ya kiungo wa Arsenal Jack Wilshere. Beki huyo aliandika katika ukurasa wake kwenye mtandao wa kijamii wa twitter kuwa hakudhamiria kucheza faulo ile kwakuwa wote walikuwa na nia ya kufuata mpira hivyo suala la kugongana lilikuwa haliepukiki. Naye kocha wa City Roberto Mancini alipoulizwa kama wataka rufani juu ya adhabu ya mechi tatu aliyopewa beki wake huyo alijibu kuwa watafanya hivyo kwakuwa tukio lenyewe halikuwa baya kama lilivyoonekana mara ya kwanza.

No comments:

Post a Comment