Balotelli mwenye umri wa miaka 22 baadae alionyeshwa akitenganishwa na Mancini huku akiwa ameshikwa na ofisa mmoja wa timu hiyo ikiwa ni tukio la kushangaza wakati City ikijiandaa na mchezo wa mzunguko wa tatu wa Kombe la FA dhidi ya Watford. Mancini alichukia kufuatia Balotelli kumchezea vibaya mchezaji mwenzake anayesadikiwa kuwa Scott Sinclair katika mazoezi hayo ambapo kwa mara nyingine tukio hilo linamuweka nyota huyo katika mlango wa kutokea. Tukio hilo limekuja ikiwa ni siku moja imepita toka mchezaji mwenzake wa zamani katika klabu ya Inter Milan, Zlatan Ibrahimovic kudai kuwa Balotelli ndio chaguo sahihi kwa City katika kutetea taji lao la Ligi Kuu nchini Uingereza.
No comments:
Post a Comment