Tuesday, January 8, 2013
Miroslov Stoch - Puskas Award
KOCHA wa timu ya taifa ya Hispania, Vicente del Bosque ameteuliwa kuwa kocha bora wa mwaka 2012 na kuwashinda Jose Mourinho wa Real Madrid na kocha wa zamani wa Barcelona Pep Guardiola katika sherehe zilizofanyika jijini Zurich, Switzerland. Del Bosque ambaye ameiongoza Hispania kutwaa ubingwa wa dunia pamoja na kufanikiwa kutetea taji lake la michuano ya Ulaya ameshinda tuzo hiyo kwa mara ya kwanza baada ya kuipoteza kwa miaka miwili mbele ya Mourinho.Mbali na tuzo hiyo pia mwanadada Abby Wambach wa Marekani alinyakuwa tuzo ya mchezaji bora wa mwaka kwa upande wa wanawake baada ya kuisaidia nchi yake kunyakuwa medali ya dhahabu katika michuano ya Olimpiki iliyofanyika London. Bao bora la mwaka lililopata tuzo katika sherehe hizo lilikuwa ni la mchezaji wa zamani wa Chelsea ambaye kwasasa anacheza katika klabu ya Fenerbahce ya Uturuki, Miroslav Stoch ambaye alifunga bao la tik-tak katika mchezo dhidi ya Genclerbirligi katika Ligi Kuu nchini humo maarufu kama Super Lig.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment