WINGA machachari wa kimataifa wa Ureno, Ricardo Quaresma anatarajia kuondoka katika klabu ya Besiktas ya Uturuki baada ya kukubali kujiunga na klabu ya Al Ahli ya jijini Dubai kwa mkataba wa miezi 18. Katika taarifa iliyotolewa na magazeti ya huko Quaresma mwenye umri wa miaka 29 ambaye amewahi kucheza katika vilabu cya Barcelona, Inter Milan na Chelsea anatarajia kuziba pengo la kiungo wa Nigeria Achille Emana ili kutimiza idadi ya wachezaji wanne wa kigeni wanaohitajika katika klabu hiyo. Ofisa Mkuu wa klabu hiyo Ahmed Khalifa alithibitisha juu ya uhamisho wa mchezaji huyo na kudai kuwa ni mara chache kupata mchezaji wa kiwango cha juu kama Quaresma ingawa alikataa kutaja mambo waliokubaliana katika mkataba. Besiktas ilisitisha mkataba wa miaka mitatu wa Quaresma ikiwa imebakia miezi sita kufuatia kuzozana na meneja wa klabu hiyo Carlos Carvalhal wakati wa mechi ya michuano ya Europa League Machi mwaka jana.
No comments:
Post a Comment