Friday, February 8, 2013

BERLUSCONI AVIJIA JUU VYOMBO VYA HABARI KWA KUKUZA MAMBO.

MAKAMU wa rais wa klabu ya AC Milan, Paolo Berlusconi amesema kuwa mshambuliaji nyota wa zamani wa Manchester City Mario Balotelli ameelewa kauli yake aliyotoa haikuwa na maana mbaya kama vyombo vya habari vinavyopamba suala hilo. Berlusconi ambaye ni kaka yake na rais wa klabu hiyo Silvio Berlusconi amesema Balotelli hakuumizwa na kauli yake yenye kuashiria ubaguzi aliyotoa hivi karibuni. Makamu huyo wa rais alipigwa picha za video kabla ya mchezo baina ya Milan na Udinese uliochezwa Jumapili iliyopita akiwaambia baadhi ya watu aliokuwa nao katika kikao kuwa waende wakamtazame kijana mdogo mweusi aliyekuja katika familia yao. Lakini Berlusconi ambaye alipigwa picha akitabasamu na mshambuliaji huyo kwenye mazoezi ya klabu hiyo amesema nyota huyo ameelewa kuwa kauli yake hakumaanisha suala la ubaguzi kama inavyokuzwa.

No comments:

Post a Comment