Sunday, February 3, 2013
GAZZA AHITAJI MSAADA WA HARAKA KUTOKANA NA MATATIZO YA ULEVI YANAYOMSUMBUA.
WAKALA wa kiungo wa zamani wa kimataifa wa Uingereza Paul Gascoigne maarufu kama Gazza anaamini kuwa maisha ya nyota huyo yako hatarini baada ya kuanza tena ulevi wa kupitiliza. Gazza ambaye amewahi kusumbuliwa na matatizo ya unywaji wa pombe uliopitiliza na kulazwa katika hospitali moja ya waginjwa wa akili miaka mitano iliyopita, alionekana kuwa katika hali ya kilevi wakati wa shughuli za kijamii jijini Northampton Alhamisi iliyopita. Wakala wake Terry Baker amesema nyota huyo hawezi kumshukuru kwa kusema hivyo lakini anahitaji msaada wa haraka ili kumuepusha na kadhia hiyo. Baker amesema wakati alipomuona katika mipindi kabla ya sherehe za Noel Novemba mwaka jana alikuwa yuko sawa lakini hivi sasa hali hiyo imebadilika na anadhani hata mwenyewe Gazza analijua hilo. Naye golikipa nyota wa zamani wa klabu ya Manchester United, Peter Schmeichel alikitaka Chama cha Wachezaji wa Kulipwa kuingilia kati suala hilo na kuangalia jinsi ya kumsaidia nyota huyo ambaye amewahi kucheza katika vilabu vya Newcastle United, Tottenham Hotspurs, Lazio na Rangers.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment