Monday, February 4, 2013
GERRARD MCHEZAJI BORA WA MWAKA UINGEREZA.
KIUNGO nyota wa kimataifa wa Uingereza na klabu ya Liverpool, Steven Gerrard ametajwa kuwa mchezaji bora wa mwaka wa nchi hiyo kwa ya pili. Gerrard mwenye umri wa miaka 32 ambaye ni nahodha wa Uingereza na Liverpool alikabidhiwa tuzo hiyo aliyopata kutokana na kura zilizopigwa katika mtandao wa Chama cha Soka cha nchi hiyo na Sir Bobby Charlton jijini Burton. Mshambuliaji wa Manchester United Danny Welbeck alishika nafasi ya pili katika kinyang’anyiro cha tuzo hizo huku nafasi ya tatu ikishikwa na beki wa Chelsea Ashley Cole. Akihojiwa mara baada ya tuzo hizo Gerrard amesema ni heshima kubwa kwake kupata tuzo hiyo haswa ikizingatiwa aina ya wachezaji wa nchi hiyo na ubora wao ulivyo. Wachezaji wengine ambao wamewahi kushinda tuzo hiyo mara mbili ni pamoja na kiungo wa Chelsea Frank Lampard na mshambuliaji wa United Wayne Rooney.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment