Sunday, February 3, 2013
NCHI ZA AFRIKA MAGHARIBI ZATAWALA AFCON.
MICHUANO ya Mataifa ya Afrika-Afcon inayoendelea nchini Afrika Kusini imeonekana kutawaliwa na nchi za Afrika Magharibi baada ya kuingiza timu saba katika hatua ya robo fainali. Hii ni mara ya kwanza kwa upande mmoja kuingiza timu nyingi katika hatua hiyo toka robo fainali ilipoanza rasmi mwaka 1972 baada ya kupanuka kwa mashindano hayo kufikia timu 12. Nchi saba hizo kutoka Afrika Magharibi zilizofuzu hatua hiyo ni pamoja na Cape Verde waliokuwa kundi A, Ghana na Mali waliofuzu kupitia kundi B, Burkina Faso na Nigeria kundi C na Ivory Coast na Togo kundi D. Nchi pekee ambayo haipo katika Muungano wa Soka kwa Nchi za Afrika Magharibi-WAFU na ilifaulu kufika hatua ya robo fainali ni wenyeji Afrika Kusini. Hata hivyo wenyeji hao nao wametolewa kwenye mchezo wa robo fainali uliofanyika jana kwa changamoto ya mikwaju ya penati na Ghana hivyo kubakisha nchi za upande huo pekee zikitamba kugombea taji hilo la Afcon.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment